Kampuni Ya King Lion Motorcycle Dar es salaam Tanzania Yakabidhi Gari La Matangazo Kwa Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani Kuelekea Wiki Ya Nenda Kwa Usalama.
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wamepokea gari lililotolewa na kampuni ya uuzaji wa pikipiki aina ya king lion motorcycle likalotumika katika kutoa elimu kwa njia ya matangazo na burudani kwa kutembea sehemu mbalimbali kuanzia dar es salaam kuelekea mkoani kilimanjaro ambapo ndipo kilele cha maadhimisho ya nenda kwa usalama yatakapofanyika kitaifa.
Mbali na gari hilo kampuni hiyo ya king lion wamejipanga kutoa zawadi mbalimbali zitakazo safirishwa na gari hilo ambazo zinatarajiwa kutolewa katika kilele cha maadhimisho hayo mkoani kilimanjaro.
Maoni
Chapisha Maoni