WATANZANIA NI WAKOSOAJI SANA – QUICK ROCKA


Msanii wa muziki na mtayarishaji, Quick Rocka ‘Switcher’ amedai Watanzania wengi wana tabia ya kumsubiri mtu akosee ili wamseme vibaya na sio kumshauri mapema ili usikosee.


Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Down’, amewashauri wasanii wenzake kusikiliza kazi za zamani na siyo kusubiria ushauri.
“Watanzania wengi ni wakosoaji. Wasanii wengi wanaoharibu kazi huwa wanawaogopa wakosoaji na ndiyo maana utakuta wanaangaika kutengeneza muziki wa tofauti kumbe ndiyo wanaharibu,” Rocka alikiambia kipindi cha Planet bongo ya EA Radio.
Aliongeza, “Mimi nawashauri tu kama watu wanataka muziki mzuri wasikilize nyimbo za zamani kisha wakitengeneze kazi zao yani hit song,”
Katika hatua nyingine Quick Rocka amesema wimbo wake mpya aliomshirikisha Mimi Mars ni mchanganyiko wa nyimbo nyingi ukiwemo wa ‘One dance’

Maoni