NA BONIFACE GIDEON, TANGA
Vijana wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili wapate nafasi ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama cha mapinduzi ccm.
Wito huo umetolewa na katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Tanga Lupasio Kapange wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, Kapange alisema vijana ndio tegemeo kubwa ndani ya ccm hivyo wasiwe na woga kuchukua fomu za kuwania nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho tawala.
Aliongeza kuwa ccm wilaya ya tanga imeshaanza kutoa fomu kuanzia ngazi ya kata , matawi na mashina na tayari wanachama wameshaanza kujitokeza kuchukua fomu hivyo ni vyema vijana wakajitokeza kwa wingi kuchukua fomu ''Mchakato wa uchaguzi ndani ya chama wilaya ya tanga unaendelea vyema tupo katika hatua ya utoaji fomu ngazi ya kata ,matawi na mashina tunawaomba vijana kujitokeza kwa wingi maana wao ndio nguzo ya ccm, nafasi zipo nyingi Kuanzia mashina mpaka taifa pia vijana watambue kuwa hakuna gharama yoyote'' Aliongeza Kapange
Aidha akizungumzia mchakato wa uchaguzi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Tanga, Kapange alisema mpaka sasa wameshatoa fomu kwenye kata zote na mabalozi, aliongeza kuwa hatua inayofua baada ya hapo nikufanya uhakiki.
Alisema ccm wilaya ya Tanga imejipanga kuhakikisha inasimamia mchakato wa uchaguzi na hakuna mwanachama yeyote mwenye sifa zinazokidhi vigezo vya uongozi atakayeonewa , aliwataka wanachama wanaochukua fomu za kuwania nafasi za uongozi kuepuka kutoa au kupokea Rushwa kwani wakigundulika hawatapata nafasi za uongozi ndani ya ccm.
Maoni
Chapisha Maoni