POLISI TANGA YAKAMATA PIKIPIKI 225 KWA MAKOSA YA KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI.

Displaying wakulyamba.JPG
​Kamanda  wa polisi  mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akizungumza  na  Waandishi  wa  habari( picha na Boniface Gideon )

NA BONIFACE GIDEON, TANGA

Jeshi  la police  hapa mkoani Tanga kwakushirikiana  na  kikosi cha usalama  barabarani limefanikiwa kukamata  zaidi ya  pikipiki  225 kutokana  na  makosa  mbalimbali  ya  usalama  barabarani.

Akizungumza  na  waandishi wa  habari, Kamanda wa  polisi mkoa  wa Tanga Benedict  Wakulyamba  alisema operesheni  hiyo  ya kukamata pikipiki zinazojihusisha  na Uhalifu  wa barabarani pamoja na  makosa ya usalama  barabarani  ulianza Tar. 22 April na  ilihusisha  wilaya  zote  za  mkoa  wa  Tanga.

 Aliyataja   makosa yaliyo sababisha kukamatwa kwa pikipiki  katika operesheni  hiyo kuwa  nipamoja  na Ubovu  wa  pikipiki -50 , makosa  ya kuvaa kofia ( Helmenti ) walikamata pikipiki 58 , makosa ya kutokuwa na  Bima walikamata pikipiki 42 , makosa  ya kuzidisha Abiria walikamata pikipiki 01 , makosa  ya  kuendesha pikipiki  bila leseni ( D/LICENCE ) Walikamata  pikipiki 74.

Kamanda Wakulyamba alibainisha  kuwa mara  baada  ya  kukamata  pikipiki hizo  waliweza  kuchukua  hatua  mbalimbali kutokana  na aina  ya  makosa alizitaja  baadhi  ya  hatua zilizochukuliwa kuwa  ni pamoja  na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 19 , kuwalipisha  faini watuhumiwa 15 ambapo waliweza  kupata zaidi  ya  TSH.450,000/= aliongeza  kuwa makosa  ya kutokulipa  kodi  TRA yapo 33 na  tayari yashughulikiwa na mamlaka ya  mapato  TRA  Mkoa wa Tanga, alisema pikipiki zilizoachiwa 18 huku pikipiki 184 zikiwa  zimebaki chini ya  ulinzi wa  jeshi  la  police.

Akizungumzia operesheni  hiyo  Kamanda wakulyamba  alisema kuwa operesheni  hiyo  niendelevu  katika  wilaya  zote  za  mkoa wa Tanga '' tunaendelea  na operesheni  hii  kwani wananchi  wamechoka  na  ajari  za barabarani  na  sisi   jeshi  la  police  tumejipanga  kuhakikisha tunatokomeza  ajari zinazotokana  na pikipiki maarufu kama  bodaboda wito  wangu kwa madereva  na wananchi kwaujumla kila  mmoja azingate  wajibu wake tukifanya  hivyo tutaweza  kutokomeza  ajari pamoja  na  uhalifu'' alisema kamanda  Wakulyamba.

Maoni