
PRODYUZA na muigizaji wa filamu za Kibongo, William Mtitu, amefunguka kuwa filamu za nje ziendelee kuingia nchini ila kwa utaratibu unaotakiwa kwa sababu zinatoa changamoto kwa wasanii wa filamu hapa nchini ili waweze kutengeneza kazi zenye ubora.
Akizungumza na Mtandao wa Global Publishers, Mtitu amesema kuwa hakuna sababu ya kuzipiga marufuku filamu zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi badala yake serikali iweke utaratibu wa kodi kwa kazi hizo.
“Hakuna sababu ya kukataa filamu za nje zisiuzwe nchini bali kinachotakiwa ni serikali kuzilipisha kodi ili twende sawa pia wasanii wa Bongo tunatakiwa kufanya kazi zilizo na ubora, ubunifu kwani zitauzika tu sokoni,” alisema Mtitu.

NA DENIS MTIMA/GPL
Maoni
Chapisha Maoni