KAULI YA WAZIRI MWIJAGE KUHUSU KENYA KUPIGA MARUFUKU GESI YA TANZANIA

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amekiri kupokea taarifa za katazo lililotolewa na serikali ya Kenya, juu ya uuzwaji wa gesi zinazotumika majumbani zinazotoka Tanzania na kusema wataalamu wa wizara wanaendelea kuzifanyia kazi taarifa hizo.
Waziri Mwijage ametoa taarifa hiyo wakati alipozungumza na mwandishi wa habari wa Azam Two mjini Dodoma baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo za serikali ya Kenya kupiga marufuku gesi za majumbani za Tanzania kuuzwa Kenya.
Video:

Na Emmy Mwaipopo

Maoni