ASKOFU DKT NDALIMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUZIDI KUMUOMBEA RAIS DKT MAGUFULI AWAONYA WANAOGEUZA MAKANISA MAJUKWAA YA SIASA

DSC_0031
Askofu  wa  kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalima akifaya maombi

Baadhi ya  waumini  wa kanisa hilo
mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Iringa Paul Mtakwimwa
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalimaakiwaombea  waumini wake na Taifa
Wachungaji wakiwa katika maombi
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalima akimsimika mchungaji Paul Mtakimwa na mkewe
Waumini  wakiwa katika maombi maalum
Na MatukiodaimaBlog

ASKOFU  mkuu  wa kanisa la Pentecote  Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt Rejoice Ndalima  amewataka  viongozi wa 
dini  nchini  kutumia nyumba  za ibada  kumwombea Rais Dkt John Magufuli na  kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba  hizo kusema kuumbua viongozi 
wa  serikali .

Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika  nchi hii si  ya kubenzwa makanisani na 
wachunguzaji ama viongozi wengine wa 
dini bali ni kazi ambayo inapaswa 
kuombewa  zaidi  ili 
Taifa  lizidi kubarikiwa .

Askofu  huyo ametoa kauli hiyo jana  wakati wa  uzinduzi wa kanisa ilo  Mtwivila
mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul
Mtakwimwa   ,kuwa hivi  sasa 
heshima ya  nyumba  za ibada 
imeanza kupoteza uwepo  wa Mungu 
kutokana na baadhi ya  watu  kutumia 
nyumba   za  ibada kama 
sehemu ya masengenyo na utapeli jambo 
ambalo  si  sahihi .

Alisema  kitendo  cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na wanasiasa ama vikundi vya  watu  kuishambulia serikali ama  kufanya utapeli  wa fedha
za  waumini wao kwa kuwatoza fedha  kama malipo ya huduma  wanayoitoa si
sahihi na si kazi ya  nyumba  za ibada hasa makanisa .

Pasipo  kutaja majina ya makanisa   yaliyogeuzwa majukwaa ya 
wanasiasa na baadhi ya  watu  waovu ama yanayofanya utapeli  wa 
pesa  kwa  waumini
wake ,alisema  kuwa yamezuka 
makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa
kuitwa makanisa  ili yalipaswa 
kuwa ni vyama  vya siasa ama nyumba  za
waganga  wa  kienyeji kwa maana ya  wapiga ramli .

“ Baadhi ya makanisa yamepoteza sifa ya  kuitwa ni 
makanisa maana  wanafanya  vituko vya ajabu sana  ndani ya madhabahu ya Mungu …wapo  wanaotumiwa na wanasiasa  kueneza siasa makanisani na  kila
siku  wao ni kuwa ni 
wachonganishi  dhidi ya  serikali na 
watu wake na wengine wamegeuka 
watabiri wa  uongo na watenda 
miujuzi hatarishi kwa jamii “

Alisema  kuwa kazi ya viongozi wa  dini  ni 
kuhubiri  neon ili  watu  wote  waweze kumjua Mungu na  sio kuhubiri siasa ama  kuifundisha kazi serikali ya  kufanywa wakati si  jukumu la kanisa kuwa  iwapo watu
wote  watamjua  Mungu 
watafanya kazi ya kuhudumia 
jamii  kwa  kutanguliza
hofu ya  Mungu hivyo  hakutakuwa na ufisadi , wizi ama 
watumishi  hewa hivyo kazi ya kanisa ni 
kuwafanya watu waijue kweli na kweli  iwe 
ndani ya  mioyo yao.

Askofu Dkt   Ndalima alisema kuwa kanisa   lake  limeenea 
nchi nzima na katika mkoa  wa 
Iringa  wameanzisha makanisa mawili  katika 
mji  wa Iringa na Nyololo  wilaya ya 
Mufindi ila lengo lao ni  kuhubiri 
neon la Mungu kwa usahihi na kuepuka kuwa 
kanisa la ujanja ujanja  kama  wanavyofanywa baadhi ya  watu 
wanaojiita manabii  ila kazi 
wanayoifanya  ni  sawa na manabii  wa uongo .

Akielezea  kuhusu utendaji kazi wa Rais  Dkt  Magufuli askofu  huyo 
alisema kanisa lake  linampongeza 
kwani hivi sasa nchi imekuwa na utulivu mkubwa na hakuna  tena maandamano ya  vurugu na 
kuwa kila wakati makanisa  yake
yatatenga mudu  wa  kumuombea Rais na  watendaji 
wote wa serikali na kutumia Biblia katika ibada  zake na 
sio  kutumia  matukio na kashfa  za
viongozi  kuhubiri kanisani .

Maoni