Zanzibar ina tegemea kuwa mwenyeji wa mkutano wa tatu wa watanzania wanaoishi nje ya nchi Dayasfora unaotarajia kuanza kesho ili kufanikisha malengo ya kuanzishwa kitengo cha wanadayasfora hao
Akitowa taarifa kwa waandishi wa habari Waziri wa nchi Ofisi ya raisi na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu amesema serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa na desturi toka mwaka 2014 na 2015 kufanya makongamano ikiwa ni miongoni mwa ahadi ya rais mstaafu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakayta Mrisho Kikwete.
Amesema kongamano hilo litakuwa na mafanikio makubwa kwa muitikio walioonesha kwa uwezo na upeo wa kuona katika kuhakikisha watanzania hao wanaiiunga mkono nchi yao Tanzania katika kuendeleza maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Kongamano hilo la siku mbili linatarajia kufanyika kesho na kufunguliwa na raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dokta Ali Muhammed Shein na kufungwa na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Maoni
Chapisha Maoni