VIONGOZI WA DINI KUWASHITAKI WASIOTEKELEZA AGIZO LA RAIS

mwamalangaNa Judith Mhina- MAELEZO
*Ni agizo la marufuku ya mwanafunzi atakayepata mimba kurudi shuleni,
Kamati ya Maadili yatishia kuwashitaki viongozi wa  Wilaya na Halmashauri zote nchini, kama hawata ainisha maeneo hatarishi kwa watoto wa kike na wakiume, kutokana na agizo la marufuku ya mwanafunzi atakayepata mimba kurudi shuleni.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili , Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu yote ya Dini Tanzania, Askofu William Mwamalanga, katika mahojiano na Idara ya Habari (MAELEZO).
“Nadhani viongozi  wengi bado hawajamuelewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli. Sisi kama viongozi wa dini tuliomba mambo matatu yafanyike kwao lakini hadi leo haijatekelezwa,” alisema Askofu Mwamalanga.
Mambo hayo ni pamoja na kuagiza kila wilaya na halmashauri  ipeleke mkakati wake wa kuzuia mimba shuleni na mpango kazi wake ofisi ya Waziri Mkuu au ofisi za viongozi wa dini waliopo karibu nao, utekelezaji wa mkakati huo uainishe utaratibu wa kupima mimba mabinti mara watokapo likizo.
Pia, viongozi watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo, kamati husika itawashitaki, kwa kukosa kutekeleza agizo la Rais ambalo ni la muhimu sana katika maisha ya vijana wetu, ili kujenga taifa lenye maadili na heshima ndani na nje ya Tanzania.
Vilevile, kamati inakusudia kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda, kwa ujasiri wake wa kuagiza maeneo yote ya shule yaliyojengwa nyumba za starehe ikiwemo nyumba za wageni kubomolewa mara moja.
Pongezi hizo zinatolewa kwa sababu ya ujasiri wake wa kuweza kubuni mambo ambayo ni ya msingi kwa taifa, lakini wengine wote waliopita hawakuliona hilo, pamoja na kuwa watoto wetu wa mkoa wa Dar es Salaam wameharibika kwa tabia mbaya ambazo zinaendelea katika maeneo ya shule.
Ombi la Kamati kwa Mkuu wa Mkoa ni kuangalia suala la chama kinachoendeleza wanachama wa kuoana jinsia moja, inasemekana bado kipo na kinafanya shughuli zake Dar es Salaam ingawa chama chao kimefutwa rasmi.
Akitoa mfano wa madhila ya shule za wanafunzi ambao wameshazaa iliyoko Kisumu, Kenya inayoitwa Mbali, walimu wanaoendesha mafunzo katika shule hiyo, wanachangamoto kubwa ambayo inakuwa vigumu kumaliza mitaala iliyopangwa kwa kuwa vurugu za ulezi na kuzingatia masomo inakuwa vigumu sana. 
Askofu aliongeza kwa kusema kuwa, katika Wilaya ya Rorya, watoto wengi wa kike hawaendi shule, wanaishia kutumikishwa na wavuvi katika shughuli mbalimbali kikiwemo kushiriki mapenzi na kupata ujauzito katika umri mdogo. Naomba serikali ifatilie jambo hili katika wilaya hii ambayo wazazi na walezi wa watoto hao hawajali kabisa kuangalia mienendo ya watoto wao na kujua umuhimu wa mtoto kwenda shule.
Askofu Mwamalanga alisisitiza na kuonyesha tofauti za madhila yanayotokea maeneo ya mijini ni tofauti na vijijini. Mfano mjini, watoto wengi wananyanyasika kijinsia kutoka kwa ndugu wa karibu wa familia, wadada au wakaka wa kazi majumbani, shule ambapo hukutana na watoto wenye tabia mbaya za kulawiti au kuwabaka wenzao na watu wazima ambao wana azma mbaya na watoto wa shule.
Kwa upande wa vijijini ni kutokana na mila potofu, kubakwa, kutengana kwa wazazi na kuacha watoto wanatangatanga bila uangalizi, umbali mrefu kutoka nyumbani kwenda shule, kutokuwa na mabweni kwa wasichana ambao hupanga nyumba  mitaani na kurubuniwa na wanaume, kufuata mkumbo wa marafiki wenye tabia mbaya, umaskini wa familia, tamaa ya wasichana mfano:, kula vizuri, kuvaa vizuri, starehe na mengine kama hayo.
Askofu alimalizia kwa kusema, “Nawaomba sana sana watanzania wenzangu jambo hili sio la mchezo ni lazima tulivalie njuga wote kama jamii na kulifanyia kazi stahiki kwa sasa kizazi chetu kinaelekea kubaya. Haipaswi hata kidogo kupuuza agizo la Rais ni vema tukalifanyia kazi.
Tanzania ni kati ya nchi zinazoathirika kwa kiasi kikubwa na mimba za utotoni na kusababisha mabinti wengi kukatisha ndoto zao za kupata elimu. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu, amethibitisha hilo wakati wa kupokea nyumba 50 za afya zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa – Mkapa Foundation Mkoa wa Geita amesema, “Katika   vizazi hai 100,000  akina mama 506 hupoteza maisha wakati wa kujifungua na  kati ya watoto wachanga 1000 wanaozaliwa wakiwa hai  25 hufariki dunia kati ya siku 25 hadi 28. Aidha, tatizo la mimba za utotoni limeongezeka nchini kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 27 mwaka 2016/17  hii ikiwa na maana kuwa tatizo ni kubwa.
Takwimu zinaonyesha dhahiri tukiweza kuzuia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupata mimba wakiwa shuleni, tutakuwa tumepunguza idadi kubwa ya mimba za utotoni. Maana sera ya elimu bure inamtaka kila mtoto wa Tanzania mwenye umri wa kwenda shule, aandikishwe na aanze shule.
Mzazi ambaye hampeleki mtoto wake shule sheria imeelekeza kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Hii inaashiria watoto wote kwa asilimia kubwa wapo shule , tofauti na miaka ya nyuma wakati wa uchangiaji wa elimu.
  • Ni agizo la marufuku ya mwanafunzi atakayepata mimba kurudi shuleni,
Na Judith Mhina- MAELEZO
02/08/2017

Mzazi ambaye hampeleki mtoto wake shule sheria imeelekeza kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Hii inaashiria watoto wote kwa asilimia kubwa wapo shule , tofauti na miaka ya nyuma wakati wa uchangiaji wa elimu.v

Maoni