MTANDAO WA ELIMU TANZANIA, (TenMet), WAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DARES SALAAM

Afisa Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bi. Alistidia Kamugisha, akizungumza wakati wa kikao cha kujenga ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Bloggers kilichofanyika makao makuu ya TenMet, Sinza jijini Dar es Salaam, leo Agosti 2, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BINADAMU ili aweze kuyakabili mazingira yake, moja ya nyenzo muhimu ni elimu, na kwa
kutambua umuhimu wa elimu, wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya juhudi kubwa
katika kusaidiana na serikali ili kufikia lengo la kuwapatia elimu Wananchi wa
Tanzania.
Mtandao wa Elimu Tanzania, kwa kifupi TenMet, ni moja ya taasisi zinazifanywa juhudi
kub wa katika kuhakikisha malengo yaliyotajwa hapo juu yanafikiwa.
TenMet ambayo iliasisiwa miaka 18 iliyopita ikiunganisha taasisi nyingine 39 wakati
huo, kwa sasa mtandao huo umepanuka na kufikia jumla ya taasisi 181
zilizojikita katika swala la kuhakikisha watanzania wanapatiwa haki yao ya
elimu, lakini sio tu kupatiwa elimu bali pia elimu iliyo bora.
Ili
kufikisha ujumbe kwa wahusika (jamii) TenMet hufikisha ujumbe kwa njia mbalimbali
ikiwa ni pamoja na makongamano, semina na vyombo vya habari vikiwemo vile vya
kisasa (social media kama vile Blogs).
Agosti 2, 2017, Maafisa wa TenMet waliwaalika bloggers ili kuangalia namna gani
wanavyoweza kushirikiana katika kutekeleza malengo yaliyoanishwa hapo juu ya
kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya elimu.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, alisema, lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa kikazi baina ya taasisi yake
na vyombo vya habari vya kimtandao kwani anaamini taarifa zitawafikia wadau
wengi zaidi.
“Lakini pia tunaamini ushirikiano huu utatusaidia katika kuibua changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya elimu nchini, kwa kuhabarisha umma, hivyo tunayo furaha
kubwa kukutana nanyi leo hii.”Alifafanua.
Kwa upande wake, Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha, amefafanua
kuwa, TenMet kama ambavyo malengo yake yalivyoainishwa, imekuwa ikifanya tafiti
mbalimbali kuhusu elimu hapa nchini, lakini pia kwa kushirikiana na taassi
nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuratibu mikutano, maonesho na semina kuhusu
masuala ya elimu.

Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, (katikati), akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Bi. Alistidia Kamugisha, na Afisa Programu wa taasisi hiyo, Bw. David Sizya.
 Mmoja wa washiriki wa kikao hicho, akitoa maoni yake.
 Afisa wa TenMet, Bw. Dominic Dogani, akitoa ufafanuaiz wa masuala mbalimbali yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho.
 Majadiliano yakiendelea.
 Mmoja wa washiriki wa kikao akitoa maoni yake.
 Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakinakili yaliyokuwa yakijadiliwa kupitia vitendea kazi vyao.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), Bw. Joachim Mushi, akiwa makini na yaliyokuwa yakijadiliwa.
 Mmiliki wa blog ya Jiachie, Bw. Ahmad Michuzi (kulia) akifuatilia mjadala. Kushoto ni Bw. Mushi.
 Bi. Kamugisha akiweka sawa vitabu vyenye taarifa za TenMet.
 Bw. Sizya, (kulia), akimpatia nakala ya vitabu vya TenMet mwandishi wa Mo Blog, Bw. Rabif Humwe.
Picha ya pamoja

Maoni