MAHAKAMA YA KENYA IMEWAKATAA MADAKTARI KUTOKA TANZANIA

Baada ya madaktari wa Kenya kufanya mgomo kuanzia December 2016 kwa madai ya kutaka nyongeza ya mshahara, March 18 2017 serikali ya Tanzania ilikubali kuwapeleka madaktari 500 kukabiliana na uhaba wa madaktari nchini humo, uamuzi ambao ulipingwa na watu mbalimbali hasa wananchi wa Kenya.
Leo March 31 Mahakama nchini Kenya imekubaliana na pingamizi la Chama cha Madaktari nchini humo juu ya kuajiri madaktari 400 kutoka Tanzania kwani ndani ya nchi yao kuna zaidi ya madaktari 1,400 ambao hawajaajiriwa.
Mahakama imechukulia suala hili kama jambo la haraka na kuipa Serikali muda wa siku 21 kufanya maamuzi. Mpaka sasa madaktari zaidi ya 400 kutoka Tanzania waliomba nafasi Kenya.

Maoni