Mmoja wa wacehezaji wa timu ya Lugalo Golf Club,Nicholaus Chitanda akionesha makombe aliyoyanyakuwa mara baada ya timu yao kuibuka washindi wa mashindano ya Golf yaliyojulikana kwa jina la MOSHI OPEN,yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Timu hiyo ya golf ya Jeshi ya Lugalo imewapa raha wanachama wake akiwemo Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya
Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya MOSHI OPEN.Timu
hiyo ya Golf imeirejesha heshima yake kwa wanachama na wapenzi wake kwa kuibuka na vikombe,ambapo mara ya mwisho klabu hiyo kuibuka na ushindi ilikuwa ni mwaka 2014.

Timu ya Lugalo Golf Club wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuibuka washindi wa mashindano ya Golf yaliyojulikana kwa jina la MOSHI OPEN,yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki,Mashindano hayo yalizishirikisha timu ya Ghymkana,timu ya Golf Moshi pamoja na timu ya
Gofu ya jijini Arusha.

Mmoja wa washiriki wa timu ya Lugalo Golf Club Noel Mheni akiwa mwenye furaha mara baada ya kuibuka washindi wa mashindano ya Golf yaliyojulikana kwa jina la MOSHI OPEN,yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Timu hiyo ya golf ya Jeshi ya Lugalo imewapa raha wanachama wake akiwemo Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya Moshi Open .

Maoni
Chapisha Maoni