KIDOA AAHIDIWA GARI NYUMBA NA MFANYABIASHARA DAR




 Video Queen wa Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’.

 

Wiki iliyopita tuliitambulisha ‘segment’ mpya ya Funga Ndoa na Staa ambapo tulimleta kwenu Video Queen wa Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’. 

Mlimmwagia sera ambazo tunazirusha hapa ili kama kuna ambaye Kidoa atakuwa amemuelewa basi awasiliane naye; GARI Habari! Kidoa mimi ni mfanyabiashara, sina mke, naomba uwe wangu, ninamiliki nyumba Tabata na Kivule (Dar), ukinikubali nakupa gari, nyumba na kazi zako sitakukataza kuzifanya, ninachotaka ni heshima tu. 

Naitwa Mashaka wa Dar, +255 657 486 745 MAISHA MAZURI Kidoa wewe ni mrembo mtafutaji, huna skendo kama wasichana wengine.

Nakupenda sana, sina nia ya kukuchezea bali kujengea familia bora. Naitwa Shedi wa Kinondoni, Dar, +255 657 486 745. 

KUWA MKE Kidoa, mimi ni mfanyabiashara wa mikoani, nataka uwe mke wangu wa ndoa, nikisema nakupenda itakuwa uongo hatujafahamiana ila natamani uwe wangu fanya hivyo, ukipenda tuwasiliane. 

Mimi Zungu Mweupe, +255 657 486 745 SINA KITU Kwa uzuri wako Kidoa kila anayekutazama anavutiwa nawe, natamani kuwa nawe, sina kitu bali love ya ukweli. 

Khalid wa Sinza, Dar, +255 657 486 745 NIHURUMIE Naomba uwe mke wangu, mimi ni kijana handsome, kazi yangu ni dereva, sina mke wala mtoto ila wewe ndiyo ninayekutarajia, tafadhali nihurumie uwe wangu. 

Naitwa Felix Adam, +255 657 486 745: KUTIMIZA NDOTO Nikubali Kidoa ili nitimize ndoto yangu. Naitwa Alfan Salum wa Mbezi Beach, Dar, +255 657 486 74

Maoni