Familia moja nchini Canada iliishi
na maiti katika chumba cha juu cha nyumba yao kwa miezi sita kwa kuwa
waliamini marehemu atafufuka iwapo wataendelea kumuomba mungu,lakini
mwili huo ukapatikana baada ya familia hiyo kushindwa kulipa mkopo
waliochukua kununua nyumba hiyo.
Kaling Wald mwenye umri wa miaka
50 alipatikana na makosa ya kushindwa kuwaarifu maafisa wa polisi kwamba
mumewe alifariki ,kosa ambalo na akahukumiwa kuwekwa katika muda wa
majaribio na ushauri,wakili wake alikiambia chombo cha habari cha Reuter
siku ya Jumanne.
Peter Wald mwenye umri wa miaka 52 alifariki
mnamo mwezi machi mwaka 2013 kwa kile mamlaka inasema ni sababu za
kawaida kufuatia maambukizi ya mguu wake yanayodaiwa kusababishwa na
ugonjwa wa sukari.
Mkewe Kaling Wald alimwacha kitandani na
kufunga chumba hicho katika nyumba yao ya Hamilton ,Ontario ili kuzuia
harufu kali iliokuwa ikitoka chumbani humo kuwafikia watu waliokuwa
wakiishi nyumbani humo.
Kama vile Yesu alivyomfufua Lazaro baada
ya siku ya nne ,pia yeye aliamini kwamba Mungu atamfufua mumewe wakili
wa mwanamke huyo alisema.
Maoni
Chapisha Maoni