“WANANCHI WA MUHEZA WAHAMASIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, ZAIDI YA KAYA 65 ZENYE WANACHAMA 390 WAHAMASIKA NA KUJIUNGA PAPO HAPO”

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya Potwe wilayani Muheza uliofanyika leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasiska na kujiunga
paoo hapo.
2 3MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)
wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za
msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye
mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo
linaendelea kwa muda wa siku kumi.
4Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wilayani Muheza George Mhada kushoto akipokea fedha kutoka kwa Diwani wa
Kata ya Potwe katikati Rashid Mdachi  anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) wilayani humo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye
wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.
5Msanii wa Maigizo mkoani Tanga Dr.Nyau na swahiba wake wakifanya yao kwenye uzinduzi wa wa Kampeni ya Kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) leo uliofanyika kata ya Potwe wilayani Muheza ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
zilifanikiwa kujiunga.
7Afisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)kutoka Makao Makuu Isaya Shekifu wa pili kulia akifuatilia uandikishwaji wa wanachama
wapya wa mfuko wa afya ya Jamii(CHF) leo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika Kata ya Potwe wilayani Muheza wa kwanza kulia ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe kulikofanyika uzinduzi huo,Dr.Swalehe Mudhihiri ambapo
zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.
8 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu na wafanyakazi
wa mfuko wa Bima ya Afya mkoani Tanga,viongozi wa Kata ya Potwe na
wanafunzi wa shule ya msingi kwenye Kata hiyo leo ambapo zaidi ya kaya 65
zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga. 9 Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe
wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo
pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa
afya ya jamii(CHF) leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
walihamasika na kujiunga papo hapo.

Maoni