Madaktari wa Australia wamefanikiwa
kuwarejeshea uhai wagonjwa watatu baada ya kupandikizwa moyo uliokufa
katika operesheni ya kwanza kufanyika duniani.
Madaktari katika
hospitali ya St Vincent mjini Sydney walitumia dawa ya kuzuia kuharibika
iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Moyo ya Victor Chang kwa
kupandikiza viungo kwa Michelle Gribilas,mwenye umri wa miaka 57 na Jan
Damen mwenye umri wa miaka 44, huku mgonjwa wa tatu akiendelea kupona.
Moyo
mmoja, ulisimama mapigo kwa dakika 20 kabla ya kuurejesha katika uhai,
ukiwa umewekwa katika mashine na kuuchoma dawa ya kuzuia kuharibika.
Jan Damen, mwenye umri wa miaka 44, (akiwa katika picha na mke wake Silvana) alipandikizwa moyo uliokufa na kuupa uhai.
Moyo
unahuishwa baada ya kupoteza uhai na kupandikizwa. Hospitali hiyo
inaamini asilimia 30 za watu watarejeshewa uhai kutokana na kugunduliwa
kwa dawa hii, ambayo hupunguza kiwango cha uharibifu kwenye moyo na kuwa
tayari kupandikizwa.
Kabla ya operesheni hizi,
madaktari wa moyo wamekuwa wakitumia moyo kutoka kwa watu waliokufa kwa
asilimia 100 ambao katika uhai wao walitaka viungo vyao vitumiwe na watu
wengine wenye kuhitaji, lakini sasa upatikanaji wa moyo utaongezeka
zaidi.
Dawa hiyo iliyochukua miaka 12 kuitengeneza, pia inasaidia
kuimarisha kazi ya moyo ambao unatolewa baada ya kifo (DCD) wakati
ukianzishwa kufanya kazi upya.
Bi Gribilas, ambaye amestaafu na
kuishi Campsie kusini magharibi mwa Sydney, amesema ni mtu tofauti kwa
sasa baada ya kupandikizwa moyo mpya.
Maoni
Chapisha Maoni