MANGULA AFUNGUA OFISI MPYA YA CCM-CHATO

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akifurahia jambo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akivuta utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Chato ambayo ilikua ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo.

Kijana wa Kikundi cha Ngoma cha Chato akionyesha umahiri wake wa kuzungusha ringi la Tairi la baiskeli kwenye mboni yake ya jicho hali iliyowashangaza wananchi wengi waliofika.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akihutubia wananchi wa Bwanga waliofika kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea Chato ambapo alizindua jingo jipya la Ofisi hiyo ya kisasa.

Taswira ya Jengo jipya la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Chato ambalo ilikuwa ni ahadi ya Mbunge wa Chato ambaye pia ni waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula juu ya gari akihutubia mamia ya wakazi wa Buseresere mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.

Wananchi wa Buseresere wakimsiliza Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipopita kwenda kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Mangula.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akisalimiana na baadhi ya wananchama wa CCM katika kata ya Bwanga wilayani Chato mara baada ya kusimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya CCM wilaya ya Chato.

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula kulia mara baada ya kumpokea katika kata ya Buseresere Mkoani Geita. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ndugu Joseph Msukuma

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Ofisi ya CCM wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mbunge wa Chato Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma.

Maoni