KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiwa na    Mkuu wa Magereza Nchini Zambia, Kamishna Percy Chato wakiaangalia kazi za aina mbalimbali zinazofanywa na Wafungwa wa Zambia katika  Mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia.

Kwaya ya Wafungwa wa Nchini Zambia wakitoa  Burudani ya nyimbo za Injili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia yaliyofanyika Septemba 26, 2014.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) akisalimiana na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini  Zambia, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Zambia, Mhe.  Nickson Chilangwa(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela. Maadhimisho hayo yamefanyika Septemba 26, 2014 katika Viwanja Vya Chuo Cha Maafisa Magereza Mjini Kabwe, Zambia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Zambia, Mhe. Nickson Chilangwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika(walioketi). Wa Nne kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tano kulia) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tatu kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(Picha zote na Kitengo cha Habari Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja akiongozana na Wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia kuelekea  kwenye  Jukwaa Kuu kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa Nne kulia Jukwaa Kuu) akiwa na Wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia wakipokea Salaamu ya heshima kutoka kwa Maafisa na Askari  Magereza Nchini Zambia(hawapo pichani)wakati Gwaride hilo likipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa pole na haraka katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Zambia, Kamishna Percy Chato.

Gadi Maalum ya Maafisa na Askari Magereza wa Nchini  Zambia wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo haraka katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia yaliyofanyika Septemba 26, 2014.

Baadhi ya Maafisa na Askari Magereza na wageni wengine Waalikwa wakifutilia matukio mbalimbali yaliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa na Askari Kabwe, Zambia.


Maoni