ARUSHA WAITAKA SEREKALI KUANZISHA SIKU YA FARU.

Wakazi wa jiji la Arusha waimeitaka wizara ya maliasili na Utalii kuanzisha siku ya faru hapa nchini ikuweza kuuhisha maisha ya mnyama huyo aliyehatarini kutoweka hapa nchini huku wakiitaka Serekali kuangalia suala zima la utunzaji wa maeneo ya hifadhi za akiba kabla ya upimaji wa vijiji .
 
Kauli hiyo imetolewa na Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Mnasa kwa niaba ya waziri wa utalii Lazaro Nyalandu katika kilele cha ufungaji wa wiki ya Utalii duniani kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya maonyesho ya Nanenane Themi jijini hapa huku akisisitiza kuangalia suala zima la ushoroba kwani limekuwa katika migogoro na kuwafanya wanyama kukosa maeno yao ya Asili.
 
Dc Mnasa alisema kuwa Rasilimali hizo za taifa zinahitaji kupangwa katika kuangalia hali ya kuinufaisha jamii yote kwani sekta ya utalii imekuwa ikisaidia kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini na kuwataka jamii iliyopembezoni na hifadhi kuendelea kutunza uikolojia na kuacha uchafuzi wa mazingira yanooizunguka kwa vizazi vya wanyama na faida kwa jamii.
 
Aliitaka jamii hasa wakazi wa jiji la Arusha kupenda vivutio vya utalii ikiwemo kuvitembelea na pia kujifunza kwani itasaidia kuwapatia ajira kwa kuweza kuwaelekeza wageni wanaotembelea hapa mkoani Arusha kwa shughuli za kiutalii kama sheria ya mwaka 2008 ilivyoainisha juu ya utalii wa ndani.
 
“Tuendelee kujifunza na tunaomba wananchi wote waliokaribu na hifadhi za taifa kukabiliana na changamoto ya vita dhidi ya ujangili inayoendelea kote nchini ikiwemo ya tembo na Faru wanyama waliohatarini kutoweka,pia upimaji wa vijiji ukaendana na mazingira ya uikoloia ilikuweza kuweka mapitio ya wanyama”alisema Mnasa
 
Nae Mkurugenzi wa Bodi ya utalii hapa nchini Zahoro Kimwaga alisema Mnyama faru wapo 92 hapa nchini hivyo ni mnyama pia alie hatarini kutoweka akawataka vijana kuanza mapambano ya kuhakikisha kuwa mnyama huyo analindwa kwa gharama yeyote ikiwemo kuweka maadhimio yatakayosaidia utunzaji wa wanyama hao.
 
Kimwaga alisema kuwa Tembo leo hawezi kuishi nje ya hifadhi zetu kama hapo awali sababu kubwa ni ujangili hivyo na wasihii wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona hujuma dhidi ya wanayamapori kwenye maeneo yao.
 
Alisema kuwa mapambano haya yanihitaji mashirikiano kwani jamii inayofanya matukio ya kiuhalifu hususasni ujangili tunaishi nayo na kuijua hivyo mchango wa wananchi kwenye vita ya ujangili una sehemu yake katika kufanikisha vita hiyo.
 
“Msisahau kutembelea na kuhamasisha utalii wa ndani utsaidie kuijenga nchi yetu pia suala la kujifunza ni msingi kwa wakazi wa maeneo yanaozunguka hifadhi zetu kwa ni ajira tosha,pia msiasahau utalii wa kiutamaduni kwani umekuwa ukishika kasi kwa sasa”alisema kimwaga.

Maoni