Mdau Salum Mwalimu ajitosa kuwania nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Zanzibar


Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya  Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi kuu za Chadema kisiwani humo.

Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe  wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo  Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi  ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chjama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha  fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar

Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kundi la Zanzibar akitia saini kitambu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi kuu za chama hicho Zanzibar kw alengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Maoni