Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia),
akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa mjini Dodoma
hivi karibuni. Mashirikisho hayo yamekuwa yakipambana kufa na kupona
kuhakikisha katiba mpya inatambue wasanii kama kundi maalum na pia
ilinde mali zisizoshikika yaani miliki bunifu (intellectual property).
Maoni ya mashirikisho hayo yalishatolewa katika hatua za awali za utoaji
maoni na pia kupitia mabaraza lakini kwa bahati mbaya, hayakujumuishwa
katika rasimu. Waliokaa kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa
Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, Rais wa Shirikisho la Filamu, Bw.
Simon Mwakifwamba na Makamu mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi.
Samia Suluhu Hassan. |
Maoni
Chapisha Maoni