A Kusini yalaani mapinduzi Lesotho

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Afrika Kusini inasema matukio ya himaya ya mfalme wa Lesotho, kusini mwa Afrika, yanaelekea kuwa ni mapinduzi.

Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje alieleza kuwa nchi yake haitakubali mabadiliko ya serikali ya Lesotho kinyume cha katiba.

Alitoa wito kwa kamanda wa jeshi la Lesotho awaamrishe wanajeshi wake warudi kambini.

Hapo awali waziri mkuu wa Lesotho, Tom Thabane, aliiambia BBC ameondoka Lesotho baada ya kutishwa kuwa atauwawa.
Aliongeza kusema kuwa hatua za jeshi zimeifanya serikali isiweze kufanya kazi, na ni sawa na mapinduzi.

Lakini jeshi la Lesotho limekanusha kuwa limejaribu kupindua serikali.

Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema hali sasa imekuwa shuwari katika mji mkuu, Maseru.

Lesotho ni nchi iliyozungukwa kabisa na Afrika Kusini na inaitegemea sana Afrika Kusini kwa ajira na pato

Maoni